Waziri Gwajima atoa wito usalama wa mtoto mtandaoni

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima, ametolea wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha usalama wa watoto wanapotumia mitandao hasa kipindi cha likizo kwani pamoja na maendeleo ya teknolojia kuongeza fursa, yameibua pia hatari mbalimbali kwa watoto.

‎‎Dk Gwajima ametoa wito huo alipokutana na watoto wa Shule ya Msingi Martin Luther, mkoani Dodoma, ambapo amesema kuwa utafiti wa mwaka 2022 umeonesha kuwa watoto wameendelea kukumbana na ukatili mtandaoni, ikiwemo kushawishiwa kutuma picha zisizofaa na kukutana na wahalifu wanaojificha kwenye majukwaa ya mtandaoni.

 

‎Amesema kuwa kutokana na ukweli kwamba watoto hutumia muda mwingi nyumbani wakati wa likizo, matukio ya ukatili huwa katika kiwango cha juu kwa kuwa asilimia 60 ya matukio hutokea majumbani na mara nyingi kuhusisha ndugu wa karibu.

SOMA: Jamii iunge mkono mikakati kuwalinda watoto nchini

‎Aidha, Waziri Gwajima amewataka wazazi kufuatilia matumizi ya simu na runinga kwa watoto, kuweka muda maalum wa matumizi ya vifaa vya kielektroniki, pamoja na kuwakataza watoto kulala na simu.

‎“Watoto, nawaomba msitembee maeneo yasiyo salama hasa nyakati za usiku. Msiwe na mazoea na watu msiofahamu, kwa kuwa siku hizi wapo wengi wasio na nia njema, hususan kwa watoto wa kike. Epukeni kupiga picha zinazoonyesha viungo vya siri na kuzituma kwa watu. Msitoe taarifa binafsi za kwenu au za familia. Na kabla ya kuweka chochote mtandaoni, jiulizeni: ‘Je, wazazi wangu au jamaa zangu wangeona hili, ingekuwa sawa?’” amesisitiza Dk Gwajima.

‎Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mtoto, Sebastian Kitiku, amewashauri watoto wote nchini kutumia vifaa vya kielektroniki kwa umakini na ufasaha wakiwa nyumbani, hususan kipindi cha likizo ndefu ili kuepusha hatari zinazoweza kuhatarisha usalama wao.

‎Nao wadau wa maendeleo wanaotekeleza afua za usalama wa watoto mtandaoni wameahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ili kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya aina zote za ukatili, hususan ukatili wa mtandaoni.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button