Waziri Mkuu aanza ziara ya kikazi Temeke

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 5 ameanza ziara ya kikazi katika wilaya ya Temeke, mkoani Dar es Salaam. Katika ziara hiyo Majaliwa atakagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kuzungumza na wananchi pamoja na watumishi wa umma.