Waziri Mkuu awapongeza wanariadha Geay, Simbu

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewapongeza wanaridha wa Tanzania, Gabriel Geay na Alphonce Simbu kwa kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa kupitia mchezo huo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Juni 28 bungeni jijini Dodoma wakati akitoa hoja ya kuhairisha Bunge la Bajeti ambapo amesema Tanzania ina wanariadha wengi lakini Geay na Simbu wamekuwa mfano wa kuingwa huku akiipongeza Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kuendelea kuupa nguvu mchezo huo hapa nchini.

“Nitoe msisitizo kwa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kuibua wanariadha zaidi kuwatafutia fursa katika mashindano ya ndani na nje ili waendelea kunufaika na vipaji vyao”amesema Waziri mkuu.

Gabriel Geay aliibuka na medali ya fedha katika mbio za Boston zilizofanyika nchini Marekani mapema mwaka huu, huku Alphonce Simbu akishinda medali ya Shaba katika mbio za Osaka zilizofanyika Japan.

Habari Zifananazo

Back to top button