Waziri Mkuu awasili Japan

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Mei 23, 2025 amewasili Osaka nchini Japan kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye maonesho ya kimataifa ya Osaka (World Expo 2025 Osaka).
Akiwa nchini Japan, Majaliwa atashiriki katika kongamano la biashara, uwekezaji na utalii ambalo litahusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na Japan.
Pia, Waziri Mkuu atashiriki katika Mikutano ya Uwili yenye lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Japan.
Maonesho hayo yameanza tangu Aprili 13 na yanatarajia kumalizika Oktoba 13, 2025.
HIyo ni mara ya pili kwa Japan (Osaka) kuwa mwenyeji wa maonesho hayo ya kimataifa, ambapo mara ya mwisho yalifanyika 1970 (EXPO 1970).