Waziri Mkuu Japan arushiwa bomu

WAZIRI Mkuu wa Japan, Fumio Kishida ameondolewa bila kujeruhiwa kwenye tukio la hadhara baada ya kurushiwa kile kilichoonekana kuwa bomu, katika eneo la Wakayama hii leo.

Hata hivyo mwanamume mmoja aliwekwa kizuizi katika eneo hilo baada ya kuhisiwa kuhusika na tukio hilo. Kishida alipaswa kutoa hotuba kwa vyombo vya habari vya eneo hilo.

Shuhuda mmoja alisema waliona mtu akirusha kitu, na kufuatiwa na moshi, huku mwingine akisema walisikia kishindo kikubwa hata hivyo hakuna majeruhi waliyoripotiwa.

Shirika la utangazaji la umma la Japan, NHK, lilimnukuu Kishida akisema kulikuwa na “mlipuko mkubwa” kwenye ukumbi huo. “Polisi wanachunguza maelezo, lakini ningependa kuomba radhi kwa kuwatia wasiwasi watu wengi na kuwasababishia matatizo.”

Habari Zifananazo

Back to top button