Waziri mkuu wa Ufaransa kujiuzulu

UFARANSA : WAZIRI MKUU wa Ufaransa Michel Barnier kajiuzulu leo baada ya wabunge wa mrengo mkali wa kulia na wa kushoto kupiga kura kumuondoa madarakani.
Kura hiyo ya wabunge imeitumbukiza Ufaransa katika mgogoro mkubwa wa kisiasa katika kipindi cha miezi sita.
Barnier ambaye ni mwanasiasa mkongwe ambaye aliongoza mazungumzo ya Uingereza ya kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya, Brexit, atakuwa ni waziri mkuu aliyehudumu kwa kipindi kifupi katika historia ya Ufaransa.
Wabunge waliamua hivyo baada ya Barnier kutumia madaraka vibaya kwa kutumia sehemu ya bajeti ambayo haikuungwa mkono na mamia ya watu wakiwemo wabunge.
Rasimu ya bajeti hiyo ilikuwa inataka euro bilioni 60 ili kuziba pengo katika nakisi ya bajeti. SOMA: Bunge Ufaransa lapigwa chini, uchaguzi mpya waja
Kujiuzulu kwa Barnier kutamaliza wiki kadhaa za mvutano kuhusu bajeti iliyokuwa inakandamiza kundi kubwa la wafanyakazi.