WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk Stergomena Tax amewasili mkoani Mtwara tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku tano.
Akiwa mkoani hapa, waziri huyo atazindua na kuweka Jiwe la Msingi miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu, afya na mingine.
Akizungumza mara baad ya kuwasili uwanja wa ndege mkoani hapa, Waziri Dk Stergomena amesema ziara hizo ni zile ambazo wamekuwa wakizifanya kama viongozi wa serikali maeneo yote ya Tanzania.
SOMA: Waziri Tax akutana na balozi wa Marekani
Amesema maeneo yote yatafikiwa kwa ziara za namna hiyo kikubwa ikiwa ni kujionea kazi kubwa iliyofanyika na kuwawezesha wananchi kuiona kazi hiyo iliyofanywa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.
“Lakini pia kupata fursa ya kuongea na wananchi na sisi pia kupata mrejesho wao ili yale ambayo wanafikiria tunahitaji kuyafanyia kazi zaidi basi tutayafanyia kazi zaidi,” ameongeza.
Amesema: “Ndio madhumuni ya uwepo wangu hapa najua mtanipa taarifa na nitatembelea miradi mbalimbali na mengi tutasema wakati tukitembea maeneo mbalimbali.”
Comments are closed.