Wenyeviti mitaa wafundwa utumishi kwa wananchi

DAR ES SALAAM: CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) kimewataka wenyeviti wa serikali za mitaa waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika Novemba Mwaka jana kutanguliza huduma na utumishi kwa wananchi wao, kwani waliomba utumishi na wawakiwakilishe chama kama walivyoaminiwa.

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla ameeleza hayo leo Machi 4, 2025 wakati akizungumza katika mkutano wa viongozi wa chama na jumuiya ngazi ya shina, tawi, kata na wilaya katika Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tano katika mkoa huo.

Makalla ambaye pia ni mlezi wa Mkoa wa Dar es salaam amepongeza jitihada kubwa zilizofanyika katika uchaguzi wa serikali uliopita na kufanikisha chama hicho kupata ushindi wa mitaa 163 kasoro mmoja ambayo ni sawa na asilimia 99.9 katika mkoa huo.

Aidha, Makalla amesisitiza kuwa wenyeviti hao waliopata kuubeba utumishi vtema na kuwatumikia wananchi na kuwataka kutosimamia na kutotumia mihuri kujipatia fedha kutoka kwa wananchi.

“Nafasi mlizozipata sio za kwenu mmepewa kwa ticket ya chama cha mapinduzi ili mkawatumikie wananchi wenu, mmepata ushindi nendeni mkakiwakilishe Chama Cha Mapinduzi vizuri na kwa ukubwa wake zifanyeni ofisi zenu kuwa kimbilio la wananchi,” amesema Makalla.

Ameongeza: “Mkawe sehemu ya utumishi kwani mliomba utumishi wananchi wanawahamia tangulizeni utumishi na huduma kwa wananchi wenu bebeni utumishi wa kuwatumikia wananchi, nitashangaa mwenyekiti anayesimamia mwananchi alipe muhuri ili apate huduma”.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button