WFP waikabidhi serikali kituo msaada wa chakula

SHIRIKA la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limekabidhi kwa serikali ya Tanzania kituo cha kimkakati cha Isaka Wilaya Kahama mkoani Shinyanga kilichowekwa kwa ajili ya kugawia chakula cha msaada wakimbizi kwenye nchi za ukanda wa Magharibi.

Kituo hicho chenye eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 29,450 serikali iliwapatia tangu Januari mwaka 1996 na mwaka 2004 ilithibitisha kwa barua kupokea kwake na mwaka 2024 imekabidhi rasmi.

Advertisement

Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Chakula Duniani, Christine Mendes amesema hayo wakati wa makabidhiano rasmi na katibu tawala wa wilaya ya Kahama Hamadi Mbega kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo, Mboni Mhita.

Mendes amesema kituo cha Isaka kilijengwa na WFP kwa madhumuni ya kusambaza chakula cha Msaada kwa wakimbizi ambapo chakula hicho kilikuwa kikisafirishwa kutoka Bandari ya Dar-es Salaam kupitia reli kati.

Mendes amesema chakula walichokuwa wakisambaza zaidi ni Maharage,Mahindi na Mtama na kwa kupitia na kupeleka kwenye nchi za Rwanda,Burundi,Kongo, Kenya ,Sudani Kusini na Uganda.

“Kituo hicho kilijengwa bure na WFP nakuweka mtandao wa miundombinu ya reli mbili za kutoka Stesheni ya Isaka hadi kwenye kambi hiyo yenye umbali wa mita 1200 waliweka Maghala 54 ya kuhamishika ,uzio,nyumba mbili za watumishi na Mashine “amesema Mendes.