WFP yakabidhi vifaa vya mawasiliano OWM

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limekabidhi vifaa vya mawasiliano katika Ofisi ya Waziri Mkuu (OWM) ambavyo vitatumika katika kukabiliana na maafa hapa nchini.

Msaada huo unaohusisha ndege zisizo na rubani (drones) unathamani ya Sh milioni 102.7 na umepokelewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma, Ummy  alisema vifaa hivyo vitawezesha Ofisi ya waziri mkuu  kutekeleza shughuli za uratibu na  udhibiti  wa maafa  mbalimbali hasa katika kuchukua taarifa  katika picha ili kupata  majanga na madhara pindi yanapotokea katika nyanja za sekta na taasisi za serikali.

Ummy alieleza kwamba vifaa hivyo ni muhimu kwa kuzingatia jukumu kuu la Ofisi ya Waziri Mkuu ambalo ni Uratibu wa shughuli za Serikali  na uratibu wa shughuli za maafa na taasisi zisizo za kiserikali kwa njia ya mtandao.

 “Kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, tunaishukuru WFP  binafsi na shirika la WFP kwa kutupatia vifaa hivi muhimu kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano kwa njia ya mtandao, kufanya operesheni za utafutaji na uokoaji, kupata ramani za hatari zilizopo, uwezekano wa kuathiriwa na janga na uwezo wa jamii husika,”Alisema Mhe. Ummy.

Aidha aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais, Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kushirikiana na Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ambayo yamekuwa yakiiunga mkono Serikali katika miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi na Taifa.

Awali akimkaribisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu )  Ummy Nderiananga, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dk. John Jingu alibainisha kwamba  Ofisi ya Waziri Mkuu iko tayari kushirikiana na  (WFP) kwa kila eneo ambalo watahitaji ushirikiano huku akiahidi vifaa hivyo kutumika kama ilivyokusudiwa.

 “Tunakumbana na maafa mengi na huwa inachukuwa mda mrefu kwa waokozi au upataji wa taarifa unachelewa hivyo,kwaajili ya hizi drone naamini ufanyaji kazi na upatikanaji wa uhalisia wa tukio utapatikana kwa uraisi”.

Aidha  Mkurugenzi Mkazi Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bi. Sarah Gibson alifafanua kuwa mradi huo  ni endelevu kwa miaka mitano kuanzia Julai 2022 hadi Juni 2027 na kwamba Shirika litafanya kazi zake kulingana na viupembeel vya serikali na kuwekeza katika kilimo, elimu, maafa pamoja na wakimbizi.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button