WGC kuisaidia Tanzania kuongeza thamani ya madini

DAR ES SALAAM: Wizara ya Madini imefanya mazungumzo ya kimkakati na World Gold Council (WGC) kwa lengo la kujadili namna baraza hilo litakavyoweza kuisaidia Tanzania kuvutia uwekezaji zaidi, hususan katika eneo la uongezaji thamani wa madini yanayopatikana nchini.

Mazungumzo hayo yameongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, kwa kushirikiana na Mawaziri wa kisekta, ambapo walikutana na Mkurugenzi Mtendaji wa WGC, David Tait.

Katika kikao hicho, Serikali ilisisitiza msimamo wake wa kutokubali kusafirisha dhahabu ghafi nje ya nchi, ikieleza kuwa mkakati huo unalenga kuvutia uwekezaji katika viwanda vya kusafisha na kutengeneza bidhaa za dhahabu hapa nchini. Hatua hiyo inalenga kuongeza ajira, mapato ya ndani na mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa taifa.

Pande zote pia zilijadili kwa kina namna ya kukuza sekta ya dhahabu ili iweze kuchangia zaidi katika maendeleo ya nchi. Kipaumbele kiliwekwa katika urasimishaji na uwezeshaji wa wachimbaji wadogo, ambao wanachangia takribani asilimia 40 ya uzalishaji wa dhahabu nchini. Serikali imeeleza mpango wake wa kuwawezesha wachimbaji hao kufanya kazi kwa tija, kwa kuzingatia kanuni za usalama, utunzaji wa mazingira na uendeshaji wa kisasa.

Aidha, WGC imeonesha kuvutiwa na mfumo wa Tanzania wa usimamizi wa sekta ya madini na kuichagua nchi hiyo kwa ushirikiano maalum wa kukuza sekta ya dhahabu. Kupitia ushirikiano huo, baraza hilo litasaidia kuwajengea uwezo, maarifa na teknolojia wachimbaji wadogo ili Tanzania iweze kuwa kitovu (hub) cha mfano wa maendeleo ya sekta ya dhahabu barani Afrika.

Kutokana na Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tano zinazoongoza kwa uzalishaji wa dhahabu barani Afrika, WGC imeeleza utayari wake wa kushirikiana na Serikali katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na kuwainua wachimbaji wadogo, ambao licha ya mchango wao mkubwa, bado wanakabiliwa na changamoto za vifaa duni, ukosefu wa taarifa za kijiolojia na ugumu wa kupata mikopo kwa ajili ya mitaji.

Akitoa maelezo yake, Mtendaji Mkuu wa WGC David Tait amesema Tanzania inafanya vizuri kushirikiana na wachimbaji wadogo na kwamba WGC wapo tayari katika kushiriki kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo kwenye mnyororo mzima wa uzalishaji wa dhahabu pamoja na upatikanaji wa soko la uhakika la madini kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Baraza.

kwa upande wake Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema mpango wa kuwawezesha wachimbaji wadogo utaleta tija na manufaa makubwa kwa kuwa kwa hivi sasa mchango wao katika kukuza uchumi kupitia madini umeongezeka sana.

Mawaziri wengine walioshiriki katika mazungumzo hayo ni Waziri wa Madini, Anthony Mavunde; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka; pamoja na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com

  2. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…

    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button