WhiteCap Crisp: SBL sasa yaja na chaguo la vijana chaguo

Dar es Salaam: Kampuni ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imezindua rasmi WhiteCap Crisp, bia ya kiwango cha juu yenye kilevi kidogo ikikenga zaidi vijana.
Katika tukio lililofanyika jijini Dar es Salaam likiwakutanisha waandishi wa habari, watu maarufu mitandaoni, wapenzi wa burudani, na wadau wa chapa katika siku hiyo isiosahaulika.
Uzinduzi huu umeleta aina mpya ya bia nchini Tanzania — WhiteCap Crisp, bia iliyotengenezwa kwa ustadi na yenye kiwango cha kilevi cha 3% pekee, ikiwalenga wanywaji wa kisasa wanaotaka kufurahia muda wao kikamilifu bila kuchoka.
WhiteCap Crisp ni bia safi, nyepesi na ya kuburudisha, inayofaa zaidi kunywewa ikiwa imepozwa hadi nyuzi joto 6°C — ikitoa ladha laini na iliyo nzuri. Ni bia kwa wale wanaothamini wepesi bila kupoteza ubora, na uburudishaji.
Tukio hili liliandaliwa kuingiza wageni katika mfumo wa maisha wa #KeepingItCrisp — mfumo unaolenga uwiano, umoja katika kijamii, na ladha ya hali ya juu.
Baadhi ya wageni maalum walikuwa wanachama wa Rotary Clubs, vikundi vya wakimbiaji, wadau muhimu wa chapa na wapenzi wa burudani ambao wanashabihiana na maadili ya chapa hii — uwazi, ustaarabu, na kujitambua.
Tukio la kipekee katika usiku huo lilikuwa ni kuwasilishwa kwa WhiteCap Crisp kutoka kilele cha Mlima Meru, jambo lililoweka alama kubwa katika simulizi ya chapa — “kutoka mlimani hadi kwenye glasi.”
Wageni pia walifurahia kuonja bia moja kwa moja, uzoefu wa chapa uliobuniwa kwa ustadi, na michezo ya chapa iliyoangazia wepesi na uburudishaji wa WhiteCap Crisp.
Imetengenezwa kwa Ajili ya Mnywaji Anayejitambua
“Bia si kinywaji tu — ni sehemu ya utamaduni wa Tanzania unaoendelea kubadilika,” alisema Henry Esiaba, Mkurugenzi wa Masoko na Ubunifu wa SBL. “WhiteCap Crisp ni zaidi ya bia; ni mustakabali wa maisha ya kijamii ya Mtanzania wa kisasa. Imetengenezwa kwa ajili ya wale wanaothamini ubora kuliko wingi, utulivu kuliko vurugu, na uwepo kuliko shinikizo. Hii ni bia ya kufurahia kikamilifu huku ukibaki makini, imara, na mtanashati.”.
Kwa kiwango chake cha chini cha kilevi, mchakato wa utengenezaji wa hali ya juu, na ladha ya kuburudisha, WhiteCap Crisp inalenga Watanzania wenye umri kati ya miaka 25 hadi 40 — wanaopenda maisha ya kijamii, wanaojali afya, na wanaochagua kwa makini wanachotumia ili kubaki na uthabiti katika maisha yao ya kila siku.
#KeepingItCrisp Imeanza Hapa
Kadri WhiteCap Crisp inavyoendelea kusambazwa kwenye maeneo ya starehe jijini Dar es Salaam, tukio hili la uzinduzi linaweka msingi wa chapa hii mpya — chapa inayolenga kubadilisha mtazamo wa Watanzania kuhusu unywaji wa bia.
Kwa kusisitiza uzoefu wa hali ya juu, burudani ya kujitambua, na uhalisia wa kijamii, WhiteCap Crisp inaleta mapinduzi katika utamaduni wa bia.