BUNGE la Tanzania, limepitisha bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ya jumla ya Sh bilioni 383.
6.
Kati ya fedha hizo shilingi bilioni 5.5 ni kwa ajili ya Tume ya Utumishi wa Mahakama, shilingi bilioni 19 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, shilingi bilioni 17 Kwa ajili ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na shilingi bilioni 68.7 kwa ajili ya Ofisi ya Taifa ya mashtaka.
Waziri wa Katiba, Dk Damas Ndumbaro akiomba idhini ya bunge kupitisha bajeti hiyo alisema kati ya fedha hizo shilingi bilioni 217.9 ni kwa ajili ya mfuko wa Mahakama.