WIZARA ya Afya Tanzania na Wakala wa Maendeleo Afrika (AUDA NEPAL) leo wamesaini mkataba wa ushirikiano katika maeneo matano ya afya ikiwemo afya ya uzazi kwa vijana walioko shuleni.
Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amesema wakala huo uko tayari kutoa kiasi cha Sh bilioni 2.71 kufanikisha zoezi hilo ambalo mchakato wake utaanza mwezi Oktoba,2024.
Maeneo mengi aliyoainisha Waziri Mhagama ni Bima ya Afya kwa wote utekelezaji wa kuwa na wahudumu wa afya ngazi ya jamii wawili kwa kila mitaa na kitongoji.
“Eneo lingine ni Mamlaka ya Dawa na Vifaa (TMDA): “Tunataka kuweka mifumo zaidi kusimamia wametoa Dola 300,000 tunasimamia kuhakikisha malengo yanafanikiwa hapa tukifanya vizuri bidhaa za afya zitakuwa hazina maswali,”amesisitiza
Amesema eneo lingine ni la afya ya uzazi kwa vijana katika shule za sekondari kuepuka mimba zisizotarajia na kuboresha vituo vya afya ya uzazi na kuokoa maisha ya watoto wachanga.
Waziri Mhagama ameeleza kuwa eneo lingine ni kutapambana na unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto na kutumia akili mnembe katika sekta ya afya hali itakayosaidia wataalamu kushirikiana kwa haraka na minyororo mingi kama dawa,tiba na mengine kufikika kwa urahisi.
“Tumejadiliana namna ya kufanya ushirikiano na tutapata fedha ambazo sio mkopo kupiga hatua tunamshukuru kwa kutuunga mkono sisi na wamesema Rais mwanamke anafurahisha na jinsi anavyoongoza nchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Maendeleo Afrika (AUDA NEPAL) Nardos Bekele amesema wametenga kiasi cha Dola milioni 100 kwaajili ya miradi mbalimbali Afrika.
“Tunayo furaha tuko hapa kushirikiana nanyi tunaunga mkono mnachofanya mwisho wa yote tutapanua uchumi wa Afrika ili kuwa na uchumi mkubwa Kwa pamoja tunahakikisha kila uungwaji mkono kwa Afrika unazaa matunda,” amesisitiza.
Amesema Tanzania imefanya mambo mengi hasa wakati huu wa uongozi wa Rais Samia wakithamini zaidi sekta ya afya na wanaunga mkono eneo la madawa Afrika kwani ni sehemu muhimu ya taifa.
“Tutaendelea kuwekeza Tanzania na tunataka kuona fedha zitakazotolewa zitaleta mafanikio tuna dola milioni 100 (Sh Trilioni 2.7)na Tanzania itapata dola milioni moja kama wakifanya vizuri wataongezewa.