Wagonjwa 823 kufanyiwa upasuaji macho

JUMLA ya  wagonjwa 823 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho katika kambi maalum ya madaktari bigwa iliyowekwa na Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya ‘Helen Keller International’ na wadau wengine wa sekta ya afya.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Igunga ,Elizabeth Rwegasila amesema hayo leo wakati wa ufunguzi wa kambi ya madaktari bingwa wa macho iliyowekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha afya ya macho na kuondoa tatizo la upofu kwa wananchi ambapo macho  996 yamefanyiwa uchunguzi.

“Idadi hii inaonesha ukubwa wa mahitaji ya huduma za macho kwa wananchi wa eneo hili, wanaonufaika na huduma hiyo wanapatiwa huduma mbalimbali muhimu ikiwemo usafiri kutoka majumbani mwao, malazi, chakula pamoja na huduma za matibabu kabla na baada ya upasuaji,” amesema  Rwegasila

Aidha, amelishukuru Shirika la Helen Keller International kwa kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha huduma za afya ya macho, akieleza kuwa mbali na kutoa huduma za matibabu, shirika hilo limechangia kuwajengea uwezo wataalamu wa afya ili kuendeleza huduma hizo hata baada ya mradi kukamilika.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Wizara ya Afya Dk Greater Mande amesema mtoto wa jicho ni miongoni mwa sababu zinazosababisha upofu kwa wananchi wengi, kupitia kambi hiyo wagonjwa wengi wamepata fursa ya kurejeshewa uwezo wao wa kuona na kuendelea na shughuli zao za kila siku.

Pia, Dk Mande amewahimiza wananchi watakaonufaika na huduma hizo kuwa mabalozi kwa jamii zao kwa kutoa taarifa kwa watu wengine wenye changamoto za macho ili waweze kujitokeza kupata matibabu wanapopata fursa hiyo.

Nae, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dk Boniface Marwa amesema wataendelea kushirikiana na wadau ili huduma hiyo ya upasuaji na mtoto wa jicho inakua endelevu na wananchi waendelee kupata huduma hizo pamoja na kuwashukuru Helen Keller kwa kuwasimesha wataalam wa eneo hilo. SOMA: Mloganzila wafanya upasuaji wa makengeza, vifuniko vya macho

Sambamba na hilo, Mkurugenzi wa Shirika ka Helen Keller International Dk Geogle kabona amesema msaada huo utaendelea kutolewa pamoja na kutoa huduma ya mafunzo kwa wataalamu wa eneo hilo pamoja na kutolewa kwa elimu ili jamii ipate uelewa huo. “Tutaendelea kushirikiana na Serikali katika juhudi za kupunguza upofu unaozuilika na kuhakikisha wananchi wengiz zaidi wanaoata huduma bira za afya ya macho,” amesema Dk Kabona

 

Habari Zifananazo

One Comment

  1. ★彡[𝐍𝐄𝐄𝐃 𝐏𝐄𝐎𝐏𝐋𝐄 𝐅𝐎𝐑 𝐏𝐀𝐑𝐓 𝐓𝐈𝐌𝐄 𝐎𝐍𝐋𝐈𝐍𝐄 𝐖𝐎𝐑𝐊]彡★

    I get paid over $220 per hour working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $35,000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by visiting Following Link…
    .
    You can check more……………… https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button