Wizara ya Nishati yashiriki tamasha Kizimkazi Zanzibar

WIZARA ya Nishati imeshiriki tamasha la Kizimkazi (Kizimkazi Festival) linaloendelea katika kijiji cha Kizimkazi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Kisiwani Zanzibar.

Wizara hiyo na taasisi zake zimetoa elimu ya utekelezaji wa Sera ya Nishati ya mwaka 2015 na kutoa huduma ya utekelezaji wa mkakati wa taifa kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa mwaka 2024-2034.

Katika Banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wananchi wameweza kujionea moja kwa moja shughuli za uchimbaji wa gesi asilia, usafirishaji na uchakataji wake kupitia teknolojia ya uhalisia pepe ‘Virtual Reality’ pamoja na kuelezwa juhudi za serikali katika uendelezaji wa sekta ya mafuta na gesi asilia.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)

Banda la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), wananchi wamejionea  utekelezaji wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere ( JNHPP) ambao umekuwa kivutio kikubwa  kupitia kifaa cha uhalisia pepe, sambamba na kutoa elimu juu ya mchango wa Tanesco katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kutoa elimu ya matumizi bora ya umeme.

Banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wananchi wanapata huduma moja kwa moja za nishati safi ya kupikia kupitia wadau wa usambazaji na waendelezaji wa teknolojia husika, elimu ya usambazaji umeme vijijini na vitongojini na uendelezaji wa miradi ya umeme.

Taasisi nyingine za Wizara ya Nishati zinazoshiriki Tamasha hilo ni pamoja na Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli ( PURA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ambao wanatoa elimu kwa umma kuhusu shughuli za udhibiti.

Habari Zifananazo

Back to top button