Wizara ya Uchukuzi yaomba bajeti Tril.2.7

DODOMA: WAZIRI wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ameliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya zaidi ya Shilingi Trilioni 2.746 kwa ajili ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya wizara hiyo jijini Dodoma, Profesa Mbarawa amesema kati ya fedha hizo, zaidi ya Shilingi Bilioni 125 zinatengwa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na zaidi ya Shilingi Trilioni 2.6 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.

“Katika fedha za Matumizi ya Kawaida, zaidi ya Shilingi Bilioni 96 ni kwa ajili ya Mishahara ya Watumishi na Shilingi Bilioni 28 kwa ajili ya Matumizi Mengineyo,” alisema Profesa Mbarawa.

Kwa upande wa fedha za maendeleo, Profesa Mbarawa alieleza kuwa zaidi ya Shilingi Bilioni 2.452 zinatokana na fedha za ndani, Shilingi Bilioni 168 kutoka vyanzo vya nje, na Shilingi Bilioni 533 ni mikopo na misaada kutoka nje ya nchi.

“Fedha hizi zitaelekezwa katika uboreshaji wa miundombinu ya sekta ya uchukuzi ili kuongeza ufanisi na kuchochea maendeleo ya uchumi wa nchi,” alifafanua.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button