Wizara yasifu hali ya amani, utulivu

DODOMA; WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesema Tanznaia imeendelea kuwa na hali ya amani na utulivu kutokana na ushirikiano uliowezeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama nchini.
Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Mei 25, 2026 na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2026/27.
“Katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao, wizara kupitia Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama imeendelea kufanya doria, misako na operesheni ili kubaini, kuzuia na kutanzua uhalifu.
“Ushirikiano huo umewezesha nchi yetu kuendelea kuwa katika hali ya amani na utulivu, hivyo kuwezesha raia kufanya kazi zao za kiuchumi na kijamii.
“Aidha, elimu kwa umma kuhusu utekelezaji wa falsafa ya Polisi jamii inaendelea kutolewa,” amesema Waziri Katambi



