DAR ES SALAAM; WAKATI huduma za awali usafiri wa treni za abiria katika Reli ya Kisasa (SGR), kati ya Dar es Salaam-Morogoro-Dodoma zikipangwa kuanza Julai 25, 2024, ratiba ya usafiri huo sasa imetangazwa rasmi.
Soma: Safari treni ya kisasa kuanza rasmi Julai 25
Taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Jamillah Mbarouk, imesema ratiba ya treni ya haraka itatoka Dar es Salaam saa 12:00 asubuhi na itatoka Dodoma saa 11;30 asubuhi, wakati treni ya kawaida itaondoka Dar es Salaam saa 11;30 jioni na Dodoma itaondoka saa 12;55 jioni.