SIO tetesi tena Yanga imeagana na kiungo Yannick Bangala ambaye muda wowote atatambulishwa Azam FC.
Taarifa iliyotolewa na Yanga leo imeeleza kufikia makubaliano na klabu hiyo juu ya kumnunua mchezajji huyo raia wa DR Congo.
Imeelezwa uhamisho huo ni baada ya Yanga kutomjumuisha kwenye kikosi kilichotajwa kwa ajili ya msimu ujao hata hivyo taarifa zinaeleza Bangala aliomba kuondoka Yanga siku kadhaa zilizopita.
Usajili huo utakuwa wa pili kwa wachezaji kutoka Young Africans, baada ya miezi miwili iliyopita kukamilisha usajili wa Feisal Salum.