IMEELEZWA kuwa mchezaji wa Yanga, Feisal Salum hajaripoti klabuni hapo kama alivyotakiwa kufanya na timu hiyo.
Ifahamike baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka TFF kutupilia mbali shauri la marejeo la mchezaji huyo, Yanga ilitoa taarifa Machi 6, 2023 ya kumtaka Feisal aripoti kambini kama mchezaji wao halali.
Akizungumza na Wasafi FM, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe amelazimika kutoa taarifa hiyo baada ya shabiki mmoja wa Yanga kupiga simu redioni hapo na kutaka kujua endapo Feisal amerejea klabuni.
Akitoa majibu ya swali hilo Kamwe amejibu kwa ufupi kwa kusema “hajaripoti”.