DAR ES SALAAM; YANGA kapigwa tena bwana! Pengine ndivyo unavyoweza kuzungumzia matokeo ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga na Tabora United uliomalizika muda mfupi uliopita Uwanja wa Azam Chamazi, Dar Salaam na Yanga kufungwa mabao 3-1.
Matokeo hayo yamekuja hata wiki moja haijatimia tangu Yanga ifungwe mchezo mwingine wa ligi hiyo kwa bao 1-0 na Azam FC kwenye uwanja huohuo.
Yanga ilicheza mechi nane mfululizo bila kupoteza mchezo wowote wala kuruhusu wavu wake kutikiswa, lakini mambo yalianza kugeuka ilipocheza na Azam na kisha leo kupoteza kwa Tabora United.