Yanga Princess yaachana na Nkoma

UONGOZI wa klabu ya Yanga SC umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na kocha mkuu wa Yanga Princess, Sebastian Nkoma.

Taarifa iliyotolewa leo Machi 28, 2023 na ofisi ya mtendaji mkuu wa klabu hiyo imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kwa sasa benchi la ufundi litakuwa chini ya Kocha Fredy Mbuna hadi mwisho wa msimu.

Kabla ya kujiunga Yanga, Nkoma alikuwa Kocha Mkuu wa Simba Queens kuanzia Novemba 2021 hadi Septemba 202

Habari Zifananazo

Back to top button