Yanga, Simba vita mbichi

VITA ya kuwania taji la Ligi Kuu Bara kwa watani wa jadi Simba na Yanga imeanza kunoga baada ya jana kushinda mechi zao kwenye viwanja tofauti.

Shangwe zilianza kwa mabingwa watetezi wat aji hilo Yanga, walokuwa wageni kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha kuikabili Coastal ambapo iliibuka na ushindi wa mabao 2-0. Benard Morrison aliiandikia Yanga bao la kuongoza katika dakika ya 4 akiunganisha pasi ya Jesus Moloko kabla ya kuujaza mpira nyavuni.

Bao la pili la Yanga lilifungwa na Fiston Mayele katika dakika ya 68 kwa kichwa na sasa amefikisha mabao mawili. Mayele alifunga bao hilo akipokea mpira wa kona kutoka kwa Djuma Shabani. Kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar. Mabao hayo yalifungwa na Moses Phiri na Dejan Georgijevic ‘Mzungu’ dakika ya 42 na 81.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi sita huku ikiwa haijaruhusu nyavu zake kuguswa katika michezo miwili mfululizo na hivyo kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo. Phiri alifunga bao lake baada ya Cleatous Chama kujaribu kupiga mpira wa adhabu kwa shuti kali nje kidogo ya 18 likagonga nguzo na kurudi kumkuta mfungaji aliyeumalizia kwa kichwa.

Hilo ni bao la pili kwa Phiri ambaye katika mchezo uliopita dhidi ya Geita alifunga. Dakika ya 66, kocha wa Simba Zoran Maki alimtoa mfungaji wa bao la kwanza Phiri na nafasi yake kuchukuliwa na Dejan, mabadiliko yaliyozaa matunda kwani ilimchukua takriban dakika 20 kuandika bao la pili. Dejan alifunga bao hilo akiuwahi mpira uliotemwa na kipa wa Kagera Sugar Said Kipao.

Hilo ni bao la kwanza kwa Dejan, aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Simba kufunga kutokana na aina ya utambulisho wake kwenye tamasha la Simba kuwa maarufu kwa siku za karibuni. Katika mechi nyingine kwenye Uwanja wa Liti Singida, Dodoma ili- fungwa mabao 2-1 dhidi ya Prisons, ikiwa ni mechi ya pili inapoteza nyumbani tangu kuanza kwa ligi.

Ligi hiyo inaende- lea tena leo ambapo Azam itakuwa nyum- bani kwenye Uwanja wa Azam Complex kucheza na Geita. Mtibwa Sugar itakuwa nyumbani Manungu kucheza na Ruvu Shooting, Polisi Tanzania itakuwa Sheikh Amri Abeid kuikaribisha KMC. Kwenye Uwanja wa Liti Singida Big Stars itaikaribisha Mbeya City

Habari Zifananazo

Back to top button