Yanga v Simba kitapigwa Des.13

DAR ES SALAAM; MIAMBA ya soka nchini Yanga na Simba itavaana Desemba 13, 2025 katika mchezo wa duru la kwanza la Ligi Kuu Tanzania Bara, mchezo utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Yanga akiwa mwenyeji.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu nchini (TPLB), mchezo huo utaanza saa 11 jioni na kwamba mchezo wa marudiano utafanyika Aprili 4, 2026.



