Yanga waikunia kichwa Mtibwa Sugar

DAR ES SALAAM:  KOCHA Msaidizi wa Yanga, Patrick Mabedi, amesema mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar utakuwa mgumu na kuwataka wachezaji wake kuwa makini ili kuhakikisha wanapata pointi tatu muhimu hapo kesho.

Yanga baada ya kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika wanarejea kwenye ligi na kesho watakutana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa KMC Complex.

“Kila mchezo una ugumu wake. Kwenye ligi lazima ushindani uwepo na tunaheshimu kila mpinzani. Tunahitaji kuwa makini sana kwenye mchezo wa hapo kesho dhidi ya Mtibwa. Kwa sasa tunachokifanyia kazi mazoezini ni kuhakikisha wachezaji wanatumia vyema kila nafasi wanayoipata,” amesema Mabedi.

Amesema anaamini kikosi cha Yanga kipo katika mwendelezo mzuri wa kiufundi, na kadri muda unavyosonga, timu itazidi kuwa bora zaidi kimbinu.

Akizungumzia hali ya mshambuliaji Prince Dube, Mabedi amesema hana shaka na uwezo wa straika huyo raia wa Zimbabwe, akisisitiza kuwa atarejea kwenye ubora wake.

“Dube amefanya mambo mengi mazuri. Nafahamu ana mzigo mkubwa mabegani mwake, lakini kwa uwezo alionao atakaa sawa. Kuna presha nyuma yake, hiyo ni kawaida kwa wachezaji wakubwa popote pale. Usipofunga lazima maswali yawe mengi, lakini ni suala la muda Dube atarejea kwenye makali yake, sina wasiwasi,” amesema.

-Amewapongeza mashabiki wa Yanga kwa kujitokeza kwa wingi katika mchezo uliopita, akiwataka waendelee kutoa sapoti kwenye mechi zijazo.

Kwa upande wake, mchezaji wa Yanga Offen Chikola, alisema kikosi kimejipanga kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kurejea kutoka kwenye mashindano ya kimataifa.

“Tumetokea kwenye mashindano ya kimataifa, tunakutana na mchezo mgumu. Hakuna namna nyingine zaidi ya kupambana kupata pointi tatu. Hatupo kileleni kwenye msimamo hivyo ni lazima tuhakikishe tunarejea juu,” alisema Chikola.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    .

    This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  3. Easy and easy job on-line from home. begin obtaining paid weekly quite $4k by simply doing this simple home job. I actually have created $4824 last week from this simple job. Its a simple and easy job to try to to and its earnings far better than regular workplace job. everyone (nhf-06) will currently get additional greenbacks on-line by simply open this link and follow directions to urge started.
    Click On This Link———>>> https://www.Homeprofit1.site

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button