KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema ari waliyo nayo wachezaji wa timu hiyo ni kiashiria tosha cha kuibuka na ushindi Jumapili dhidi ya TP Mazembe.
Akizungumza na HabariLeo, kocha huyo amesema mpaka sasa maandalizi ya mchezo huo upande wa kiufundi yamekamilika, wanabiri siku ya mchezo huo wa Kombe la Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
“Tunawaheshimu Mazembe kwa ukubwa wao, lakini hatupo tayari kupoteza pointi tatu mbele ya mashabiki wetu, naamini utakuwa mchezo mzuri na tutaibuka washindi,” amesema Kaze.