Yanga yaitumia Simba kung’ara Nigeria

WAKATI kikosi cha Yanga kikitarajia kuanza safari ya kuifuata Rivars United kesho afajiri kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika, Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema kufungwa na Simba kumewasaidia kubaini upungufu wa kikosi chao.

Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo amesema kuna mapungufu wameyabaini na tayari wameanza kuyafanyia kazi kwenye uwanja wa mazoezi kabla ya mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Rivers United.

“Mchezo dhidi ya Simba pamoja na machungu ya kufungwa, lakini ukweli imetusaidia sana kubaini mapungufu tuliyokuwa nayo sasa tunakwenda Nigeria tukiwa imara na matumaini ya kupata angalau pointi moja ni makubwa,” alisema Kaze.

Habari Zifananazo

Back to top button