Yanga yapania robo fainali Caf

RAIS wa Yanga, Hersi Said amesema wamejipanga kuweka nguvu kwenye maandalizi ya timu yao ili kufanya vizuri kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza na HabariLEO, kiongozi huyo ameeleza kuwa anajua wanapoelekea ni pagumu zaidi ya walipotoka ndiomaana wameamua kuwekeza kwenye maandalizi ya mapema ili kulipa nafasi benchi la ufundi kujenga timu ya ushindani.

“Malengo ya Yanga yalikuwa ni kufika robo fainali lakini kwa mwenendo wetu kwenye mechi za hatua ya makundi imetupa hamasa na kuona kama tunaweza kufika mbali zaidi ndiomaana tumekusudia kuongeza ukaribu na benchi la ufundi ili kutekeleza mahitaji yao na kutuandalia timu ya ushindani itakayotupa tunachokitaka huko tunapoelekea,” amesema Hersi.

Kikosi cha Yanga kimeingia kambini leo kujiandaa na mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya TP Mazembe pamoja na mechi za Ligi Kuu na Kombe la FA
Mwisho.

Habari Zifananazo

Back to top button