Yanga yapigwa faini Sh milioni 2

KLABU ya Yanga imepigwa faini ya Sh milioni 2 katika makosa mawili tofauti yanayouhusu michezo miwili ya Ligi Kuu.

Kosa la kwanza ambalo faini yake ni Sh milioni 1 ni mashabiki wake watatu kuonekana kwenye eneo la vyumba vya kuvalia katika mchezo dhidi ya Tanzania Prison ambapo ni kinyume na taaratibu za michezo, kwa mujibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF).

Taarifa iliyotolewa leo Februari 15 na TFF, imeeleza kuwa adhabu hiyo imezingatia kanuni ya 17:50 na 17:60 ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo.

Pia, Yanga imetozwa faini nyingine ya Sh milioni 1 kwa kosa la wachezaji wake kuchelewa kurejea uwanjani katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji hali iliyosababisha mchezo kuchelewa kuanza kipindi cha pili kwa dakika saba.

Habari Zifananazo

Back to top button