Yanga yawaza makundi CAF

DAR ES SALAAM: RAIS wa Yanga, Hersi Said amesema malengo klabu hiyo msimu ujao ni kufika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hersi ametaja malengo hayo leo Julai 9, 2025 alipofanya mahojiano na chombo kimoja cha habari wakati akitolea ufafanuzi swali lililohusu mipango ya Yanga 2025/2026.

“Kiukweli hatujawa na matokeo mazuri kwenye michuano ya Kimataifa kwa mfululizo miaka ya hivi karibuni kama tuliokuwa nayo hapa ndani, na mashindano ya Afrika ni mashindano ambayo yanahitaji maandalizi makubwa,” amesema.

“Tulifika fainali Kombe la Shirikisho Afrika, baadae tukafika robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu tulikuwa hatujaingia makundi kwa miaka 25 na baadae msimu huu tukaishia makundi Kwahiyo kwa msimu ujao malengo ya Yanga ni kuingia kwanza kwenye hatua ya makundi, na tukishaingia makundi tutabadilisha upepo hapo.” aliongeza.

SOMA ZAIDI

Rais Mwinyi aizawadia Yanga mil 100/-

“Tukishaingia kwa msimu wa tatu mfululizo tunatengeneza malengo mapya, tutafanya usajili ambao ni wa kimalengo na kimkakati na wachezaji watakaokuja kwa sababu watakuwa ni wenye ubora nao hawataishia Makundi”.

Yanga ndio mabingwa wa soka la Tanzania msimu huu wakiwa wametwaa mataji yote ya ndani kwa msimu uliomalizika huku wakiwa wameishia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika msimu ambao walitarajiwa kufanya makubwa kutokana na ubora wao katika soka hivi sasa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button