Yoon Suk agoma kukubali kushindwa

KOREA KUSINI : RAIS wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani,Yoon Suk Yeol ameapa kupambana hadi dakika ya mwisho sambamba na wafuasi wake kuendelea kupiga kambi katika makazi yake.

Katika taarifa yake aliyoitoa hapo jana Jumatano, Yoon amesema nchi hiyo kwa sasa ipo hatarini kutokana na nguvu za ndani na nje zinazotishia uhuru wake na shughuli za uasi dhidi ya serikali.

Yoon ametoa matamshi hayo baada ya wachunguzi kusema kuwa watatoa waranti ya kumkamata kiongozi huyo baada ya kutangaza sheria ya kijeshi mwezi uliopita.

Advertisement

Wakatihuohuo,wafuasi wake wameendelea kupiga kambi nje ya makazi ambako amekuwa akizuiliwa kwa wiki kadhaa, wakizuia juhudi za kumhoji. SOMA: KOREA KUSINI : Rais Yoon Suk avunja ukimya