Yoon Suk Yeol akwepa kuhojiwa gerezani

KOREA KUSINI : RAIS wa zamani wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol, anadaiwa kutumia mbinu isiyo ya kawaida kukwepa kuhojiwa na waendesha mashtaka kuhusu tuhuma za kuvuruga uchaguzi.
Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka Oh Jeong-hee, Suk Yeol alilala akiwa na nguo ya ndani pekee, hali iliyowafanya maafisa washindwe kumhoji kwa mujibu wa taratibu za kisheria.
Waendesha mashtaka walimjulisha rais huyo kwamba katika jaribio lijalo, iwapo atashindwa kushirikiana, watachukua hatua kwa kutumia nguvu za kisheria ili kuhakikisha mchakato wa uchunguzi unaendelea kama inavyotakiwa. SOMA: KOREA KUSINI : Rais Yoon Suk avunja ukimya
Yoon Suk Yeol alikamatwa baada ya kutangaza sheria ya kijeshi Desemba 3, hatua iliyozua machafuko ya kisiasa nchini humo na kukabiliwa na mashtaka kadhaa ikiwemo uasi na kuvuruga uchaguzi, lakini amekuwa akikwepa kuhojiwa mara kwa mara.