Zaidi ya milioni 43 wafikiwa msaada wa kisheria wa Mama Samia

WANANCHI zaidi ya milioni 43 kutoka mikoa 23, halmashauri 154 , kata 1,639, vijiji 4,897 vimefikiwa na kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia tangu ilipoanza.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro amesema hayo leo Machi 28 kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo mkoani Arusha inayoendeshwa na timu ya wanasheria kwa siku 10 kwenye halmashauri saba za mkoa huo.

Dk Ndumbaro amesema kampeni hiyo pia imesikiliza kero za wananchi milioni 2,192,372 kati yao wanaume ni milioni 1,088,455 na wanawake ni milioni 1,105,915 ikiwemo kuondoa changamoto zao kwa mmoja mmoja.

Amesema wizara hiyo imeweka mikakati na mipango endelevu ambayo ni kuanzisha madawati ya msaada wa kisheria  kwa kila halmashauri ambapo kila halmashauri kutakuwa na maofisa maendeleo ya jamii watakaohusika kutoa msaada huo lakini pia serikali imeingia  makubaliano na Chama cha Mawakili  wa Tanganyika (TLS) ikiwemo mafunzo ya watoa huduma 22,005 walipewa mafunzo ya msaada wa kisheria.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button