Zenji Boy: Midundo yetu inahitaji vionjo vya muziki wa asili

RAPA anayeshikilia tuzo ya msanii bora kijana wa mwaka 2021 katika tuzo za muziki Zanzibar, Ison Mistari maarufu Zenji Boy amewataka wasanii wenzake kuongeza vionjo vya muziki wa asili katika midundo ya nyimbo zao ili wawe na ladha yao.

Zenji Boy amesema muziki wake umekuwa na ubora wenye ladha inayokubalika kote anakotumbuiza kwa sababu muziki wake una mchanganyiko wa vionjo vya muziki wa asili.

“Watanzania tunadharau sana muziki wetu wa asili lakini muziki huo ndiyo unaopendwa katoka soko la nje kuliko muziki mwingine wowote, hivyo tunatakiwa kuchanganya katika midundo ya nyimbo zetu ili kuongeza ladha na kuleta utofauti wa muziki na muziki,” amesema Zenji Boy

Zenji Boy licha ya kuwa rapa mashuhuri ndani na nje ya Zanzibar pia ni Dj na mtayarishaji wa muzikia anayevutiwa zaidi na miziki ya asili hasa wanaopiga kundi la muziki wa asili la Kidumbaku lenye maskani yake Zanzibar.

Pia Zenji Boy anashikilia tuzo ya video bora ya wimbo wake pamoja na msanii bora wa kiume kupitia tuzo za Zenji255 za mwaka 2017/18, aidha mwaka 2020 alishinda tuzo ya Ermason.

Habari Zifananazo

Back to top button