100 hutibiwa changamoto afya ya akili kila siku

DSM; JUMLA wagonjwa 70 hadi 100 wa afya ya akili huonwa kila siku katika kliniki zilizopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na Mloganzila.

Takwimu za MNH zinaonesha kuwa takribani waraibu wa dawa za kulevya wapatao 1,000 hunywa dawa aina ya Methadone kila siku na waraibu zaidi ya 5,000 wamepata huduma hiyo tangu mradi huo ulipoanzishwa.

Aidha Muhimbili ina mpango wa kujenga kituo cha umahiri cha kutoa huduma za utengamao kwa wagonjwa wa afya ya akili, Kijiji cha Vikuruti kikichopo Kata ya Chamazi- Manispaa ya Temeke.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Prof. Mohamed Janabi katika maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili duniani ambayo hufanyika Oktoba 10 ya kila mwaka.

Prof. Janabi amesema MNH ina eneo Vikuruti lenye ukubwa wa hekari zaidi ya 160, hivyo kuna nafasi ya kutosha kujenga kituo hicho cha umahiri kwa ajili ya matibabu ikiwemo wananchi wa kawaida, ambao watahitaji muda wa pekee wa kutulia na kufanya tafakari binafsi.

Amesema kituo hicho kitakua na majengo ya kisasa ya kupumzika, mandhari ya kuvutia, miradi mbalimbali ya kimkakati kwa ajili ya kusaidia wahitaji kama sehemu ya tiba kazi ikiwa ni maandalizi ya kumrudisha kwenye jamii mgonjwa husika.

Prof. Janabi ametoa rai kwa wananchi kufahamu na kutofautisha kuwa si kila mgonjwa wa afya ya akili ametokana na pombe au dawa za kulevya.

“Wengine wanapata changamoto ya afya ya akili kutokana na sababu mbalimbali zinazowakabili na kushindwa kuhimili,”ameeleza.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Royal
1 month ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by. follow instructions on this website…….. http://Www.SmartCash1.com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x