148 mbaroni Simiyu kwa uhalifu Aprili

BARIADI, Simiyu: JESHI la Polisi Mkoa wa Simiyu linawashikilia watu 148 kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo wizi wa mali, kukutwa na bangi, mirungi, pamoja na nyara za serikali zikiwemo pembe za ndovu.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, (ACP) Edith Swebe amesema watu hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti katika operesheni ya kupambana na uhalifu pamoja na madawa ya kulevya iliyofanyika mwezi Aprili.

Soma pia: https://habarileo.co.tz/mara-wataka-majambazi-washughulikiwe-kimila/

Amesema kuwa baadhi ya watuhumiwa hao wamefikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika, huku wengine wakiwa bado hawajafikishwa kwenye chombo hicho cha kutoa haki kutokana na upelelezi kutokamilika.

Kati yao, watuhumiwa saba wamekamatwa wakiwa na dawa za kulevya aina ya mirungi na bangi, watuhumiwa sita kwa nyakati tofauti wamekamatwa wakiwa jumla ya mabunda 1160 ya mirungi yakisafirishwa kutoka wilayani Tarime mkoani Mara kwenda jijini Mwanza.

“Jumla ya magari manne yamekamatwa kuhusika na tuhuma za usafirishaji wa madawa ya kulevya hayo ambayo ni Toyota  Passo Sette yenye namba za usajiri T.961 EAM, Toyota Harrier yenye Namba za usajiri T.997 DMK, Toyota Noah Vox yenye Namba za Usajiri T.307 AMG pamoja na Toyota Probox yenye namba za usajiri T 489 EFR,” Amesema Swebe.

Ameongeza kuwa katika Kijiji cha Bushashi kilichopo Wilaya ya Maswa, mtuhumiwa mmoja amekamatwa akiwa na magunia mawili yakiwa na bangi.

Soma pia: https://www.facebook.com/Habarileogazeti/posts/pfbid02cHxQmiP3uUBDjnSbVXbMeHUr8Utz94anh1pAwoHptGvDK2kHBs2YjbfvMab6KdJHl

Kamanda Swebe amebainisha kuwa, katika Kijiji cha Nkololo kichopo Wilayani Bariadi wamekamatwa watu watatu wakiwa na Meno ya Tembo, huku katika Kijiji cha Lung’wa kilichopo Wilaya ya Itilima watu wanane wamekamatwa wakiwa na kipande cha ngozi kavu ya Nyati, Ngozi kavu ya Chui, na jino moja la Ngiri bila kuwa na vibali.

“Watuhumiwa wote waliingia kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuwauwa wanyama hao kisha kuchukua nyara hizo, ambapo upelelezi wa kesi zao umekamilika na wamefikishwa Mahakamani,” amesema.

Kamanda Swebe amebainisha kuwa watuhumiwa wengine wamekamatwa wakiwa na mali za wizi yakiwemo Magodoro mawili, spika ya radio ‘subwoofer’ aina ya Sundar moja, subwoofer aina ya Seapiano na nyingine ya Alip. Pia vimekamatwa visimbuzi vya Azam viwili na kimoja cha Star Times.

Mali nyingine alizitaja kuwa ni deki aina  ya Black Stone na SingSung, Runinga aina ya DGM Inch 32, Alitop Inch 32, Samsung Inch 42, Mobisol Inch 32, Mitungi miwili ya Gesi aina ya Oryx, baiskeli mbili na pikipiki aina ya Kinglion MC 936 DZF Chasis L7GPCKLN941792.

Habari Zifananazo

Back to top button