198 wafutiwa mashitaka kesi ya uhaini Dar

DAR ES SALAAM; MKURUGENZI wa Mashitaka (DPP) leo Novemba 25,2025 amewafutia mashitaka jumla ya washitakiwa 198 kati ya 216 waliokuwa wakikabiliwa na mashitaka ya uhaini na kula njama.

Washitakiwa hao walikuwa na kesi zilizogawanywa katika makundi matatu tofauti  kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam., huku kundi la  kwanza lililokuwa na washitakiwa 22 katika kesi namba 26388 ya mwaka 2025, washitakiwa 20 waliachiwa huru, isipokuwa  Jennifer Jovin (26) maarufu ‘Niffer’na Mika Chavala,  ambao kesi yao ilikuwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya.

Pia Washitakiwa 90 kati ya 94 katika kesi namba 26395 ya mwaka 2025 wameachiwa huru baada ya DPP kutokuwa na nia ya kuendelea kuwashitaki.

Washitakiwa hao waliachiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Hassan Makube, kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa. Washitakiwa wanaosalia  ni Daud Joshua, Joshua Thobias, Michael Maliwa na Irene Silasi.

Kundi lingine ilikuwa kesi namba 26540/2025 iliyokuwa ikimkabili Haruni Mwaisumbe, Abas Mfinanga, Abdallah Kashinje, Frank Sinduka Kulwa Ngumba na wengine 95 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hassan Makube.

Wakili wa Serikali, Titos Aron alidai DPP hana nia ya kuendelea na kuwashitaki washitakiwa 88 kati ya 100, hivyo washitakiwa 12 aliendelea kuwashitaki.

Jana DPP aliwafutia  mashitaka washitakuwa 47  kati ya 48 ambao pia walikuwa wakikabiliwa na kesi ya uhaini na kumrudisha rumande mshitakiwa mmoja.

*Imeandaliwa na Ramla Hamidu, Prisca Pances na Tatu Mwakabana

Habari Zifananazo

5 Comments

  1. The Russian army also lost 11,366 (+3) tanks, 23,620 (+5) armored combat vehicles, 34,626 (+41) artillery systems, 1,549 (+0) multiple launch rocket systems, 1,248 (+0) air defense systems, aircraft – 428 (+0), helicopters – 347 (+0), UCAVs – 83,769 (+431), cruise missiles – 3,981 (+0), ships/boats – 28 (+0), submarines – 1 (+0), vehicles and tankers – 68,006 (+84), special equipment – 4,003 (+0).

    1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
      .
      This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com

    2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  2. The Russian army also lost 11,366 (+3) tanks, 23,620 (+5) armored combat vehicles, 34,626 (+41) artillery systems, 1,549 (+0) multiple launch rocket systems, 1,248 (+0) air defense systems, aircraft – 428 (+0), helicopters – 347 (+0), UCAVs – 83,769 (+431), cruise missiles – 3,981 (+0), ships/boats – 28 (+0), submarines – 1 (+0), vehicles and tankers – 68,006 (+84), special equipment – 4,003 (+0).

  3. The Russian army also lost 11,366 (+3) tanks, 23,620 (+5) armored combat vehicles, 34,626 (+41) artillery systems, 1,549 (+0) multiple launch rocket systems, 1,248 (+0) air defense systems, aircraft – 428 (+0), helicopters – 347 (+0), UCAVs – 83,769 (+431), cruise missiles – 3,981 (+0), ships/boats – 28 (+0), submarines – 1 (+0), vehicles and tankers – 68,006 (+84), special equipment – 4,003 (+0).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button