Wachezaji 28 Stars kuingia kambini
KIKOSI cha wachezaji 28 wa timu ya Taifa, (Taifa Stars) kitaingia kambini Juni 2 kwa ajili mchezo wa kirafiki dhidi ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) na mashindano ya COSAFA dhidi ya Eswatini na Madagascar.
Wachezaji walioitwa watakaouwa chini ya kocha Hemed Suleiman ni Yakoub Suleiman, Ally Salim, Hussein Masaranga, Antony Remmy, Mirajy Abdallah, Shomari Kapombe, Lusajo Mwaikenda na Vedastus Masinde.
Wengine ni Wilson Nangu, Mohamed Hussein, Ibrahim Ame, Pascal Msindo, Alphonce Mabula, Ibrahim Abdulla, Dickson Job, Abdulrahim Bausi na Idrisa Sitambuli.
Wachezaji wengine walioitwa ni Abdulrazack Mohamed, Ahmed Pipino, Yusuph Kagoma, Sheikhan Khamis, Feisal Salum, Valentino Mashaka, Kibu Denis, Simon Msuva, Iddy Selemani, Mishano Daudi na Selemani Mwalimu.



