39 wafariki kwa moto Mexico

WATU 39 wamefariki na wengine 29 kujeruhiwa baada baada ya moto kuzuka katika kizuizi cha wahamiaji Kaskazini mwa Mexico karibu na mpaka wa Marekani. Taasisi ya Kitaifa ya Uhamiaji ya Mexico imeeleza katika taarifa yao.

Imeelezwa kuwa moto huo ni moja ya matukio mabaya zaidi kuwahi kutokea katika kizuizi cha wahamiaji nchini nchini humo. Ulitokea Jumatatu jioni katika kituo cha Ciudad Juarez, ng’ambo ya mpaka kutoka El Paso, Texas.

Ofisi ya mwanasheria mkuu wa Mexico imeezisha uchunguz katika eneo la tukio, kulingana na ripoti za vyombo vya habari.

Vinagly, mwanamke wa Venezuela, alisimama nje ya kituo cha wahamiaji, akitamani sana habari kuhusu mume wake mwenye umri wa miaka 27 aliyezuiliwa hapo.

“Alichukuliwa na gari la wagonjwa,” aliambia shirika la habari la AFP. “Wao maafisa wa uhamiaji hawakuambii chochote. Mwanafamilia anaweza kufa na hawakuambii kuwa amekufa.” Alieleza.

Tukio hilo linajiri ikiwa ni mwezi mmoja uliopita tangu baadhi ya watu wafanye ghasia katika kizuizi kikubwa zaidi cha Mexico katika mji wa kusini wa Tapachula karibu na mpaka na Guatemala. Hakuna mtu aliyekufa katika tukio lolote.

Zaidi ya makazi 30 ya wahamiaji na mashirika mengine ya utetezi ya haki za binadamu yalichapisha barua ya wazi Machi 9 ambayo ililalamikia kuharamishwa kwa wahamiaji na wanaotafuta hifadhi huko Ciudad Juarez.

Ilishutumu mamlaka kwa unyanyasaji na kutumia nguvu kupita kiasi katika kuwakusanya wahamiaji, ikilalamika polisi wa manispaa walikuwa wakiwahoji watu mitaani kuhusu hali yao ya uhamiaji bila sababu.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button