Wanajeshi 60, maafisa magereza wafutwa kazi Guinea

GUINEA imewafuta kazi zaidi ya wanajeshi 60 na maofisa magereza baada ya kiongozi wa zamani wa kijeshi Moussa Dadis Camara na wengine wawili kuvunja jela.

Camara alikamatwa tena na kurudi gerezani saa chache baada ya kuachiliwa na makomando waliokuwa na silaha nzito mapema Jumamosi.

Kando na Camara, wafungwa wengine wawili pia wamepatikana.

Advertisement

Kiongozi wa Junta Kanali Mamady Doumbouya alisema Jumapili katika amri kwamba aliwafuta kazi wanajeshi na maafisa wa magereza kwa “ukiukaji wa ajira na utovu wa nidhamu”.

Maafisa wa kijeshi waliofutwa kazi ni pamoja na mtoro Claude Pivi, Moussa Thiegboro Camara na Blaise Goumou.
Msako unaendelea kumtafuta Pivi, waziri wa zamani wa usalama wa rais katika utawala wa Dadis Camara, ambaye bado yuko huru.

3 comments

Comments are closed.