Bashungwa asimamisha watano Mbulu

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa amewasimamisha kazi Maafisa watano Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara ili kupisha uchunguzi kwa kusababishia Halmashauri hasara na matumizi mabaya ya madaraka.

buy tretiva online https://bewellct.com/images/originals/jpg/tretiva.html no prescription pharmacy

Waziri wa Tamisemi Innocent Bashungwa akitangaza kuwasimimisha kazi watumishi watano Mbulu

Watumishi hao ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Juma Ibarahim  Mavumo; aliyekuwa Kaimu mweka hazina, Ramadhani Mwakamyanda; Mweka hazina wa sasa, Respicius Kagaruki; Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA, Nyanda Komanya Msirikale na Mhasibu wa Mapato, David Assey.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari, iliyotolewa leo Septemba 28, 2022 imesema kuwa Bashungwa amechukua maamuzi hayo katika kikao cha majumuisho ya  ziara yake ya  kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ na Halmashauri ya Mji Mbulu, mkoani Manyara.

Bashungwa amesema mnamo Julai 12, 2022 aliyekuwa anakaimu ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Mbulu, David Ali Assey aliandika barua kwa Kampuni binafsi ya kukopa kiasi cha shilingi milioni 6.

buy prednisone online https://bewellct.com/images/originals/jpg/prednisone.html no prescription pharmacy

7  kwa aijli ya matumizi ya ofisi na kuelekeza fedha hiyo kuwekwa kwenye akaunti binafsi ya Davidi ali Assey ambaye ni Mhasibu wa Halmashauri.

Amesema taarifa ya  CAG ya ukaguzi wa kawaida kwa mwaka wa fedha wa 2020/21 ilielekeza Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Juma Ibrahim Mvumo achukuliwe hatua stahiki kwa kushindwa kuandaa vyema masharti ya zabuni na tangazo lake pamoja na kutofanya ufuatiliaji na uhakiki wa uhalali wa kampuni ya M/S Dicsamo Traders General Supplies Co. Ltd.

Aidha. Bashungwa amesema pia, aliyekuwa Kaimu Mweka Hazina, Ramadhani Mwakamyanda na mweka hazina wa sasa, Respicius Kagaruki wachukuliwe hatua kwa kulipa gharama za uwakala kwenye akaunti ya binafsi badala ya akaunti ya kampuni M/S Dicsamo Traders iliyopewa zabuni ya kukusanya mapato ndani ya Halmashauri kiasi cha shilingi 188,499,328.

“Taarifa ya CAG ilielekeza Afisa TEHAMA wa Halmashauri, Nyanda Komanya na Mweka Hazina, Respicius Kagaruki wachukuliwe hatua kwa kushindwa usimamia vyema Mfumo wa Mapato na kuacha mashine za kukusanyia mapato kuendelea kuwa nje ya mtandao kwa kipindi kirefu bila ufuatiliaji cha siku nane hadi 1,051.”Amesema Bashungwa

Wakati huo huo, ametoa wito kwa Mabaraza ya Madiwani kuacha tabia ya kukubali kutoa misamaha wa watumishi waliobainishwa  kwenye taarifa ya CAG kuchuliwa hatua, na kubadilisha maelezo hayo kutoa mapendekezo ya  kuwapa onyo Watumishi hao.

Habari Zifananazo

Back to top button