NEEC yapendekeza elimu ya sheria ya kodi kwa wafanyabiashara wadogo

DAR-ES-SALAAM : KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa, amependekeza kuwa wafanyabiashara wadogo wapewe elimu ya sheria ya kodi, kwani wengi wao hawana uelewa wa kutosha kuhusu haki zao na wajibu wao katika ulipaji wa kodi.

Akizungumza kwa undani kuhusu changamoto hii, Issa amesema kuwa kutokufahamu sheria za ulipaji kodi kumewafanya wafanyabiashara wadogo kutowajibika ipasavyo kwa taifa, jambo ambalo limekuwa likisababisha upungufu wa mapato kwa serikali.

“Ikiwa wafanyabiashara wadogo hawana elimu ya sheria ya kodi, wanashindwa kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi inavyostahili, na hili inachangia upotevu mkubwa wa mapato ya taifa,” alisema Issa.

SOMA: Bil 5/- kukopesha wamachinga

Aidha, Beng’i Issa ameiomba Tume ya Mapendekezo ya Kuboresha Mifumo ya Kodi kuanza juhudi za kuwaelimisha wafanyabiashara wadogo katika ngazi zote za nchi, ili waweze kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa taifa.

Habari Zifananazo

Back to top button