Sh bilioni 8 kutekeleza Jenga Kesho Iliyo Bora

MTWARA: SERIKALI imetoa zaidi ya Sh bilioni 8 kwa Bodi ya Korosho (CBT) ili kutekeleza programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) kupitia zao hilo.

Mkurungezi wa CBT, Francis Alfred amesema pesa hizo zimewezesha bodi hiyo kuajiri vijana 500 maofisa ugani kilimo kutoa huduma za kilimo kwa wakulima wa korosho, elimu ya mbinu za kisasa kuzalisha korosho ili kuongeza tija kwenye uzalishaji wa zao hilo nchini.

Alfred amesema hayo leo katika hafla ya kukabidhi pikipiki na vishikwambi kwa vijana 245 maofisa ugani ambao watatoa huduma za kilimo kwa wakulima wa korosho Mtwara.

“Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) katika zao la korosho itagharimu zaidi ya Sh bilioni 8, fedha hizo zimetolewa na serikali kutekeleza mpango huo kwa muda wa mwaka mmoja,” amesema.

Amesema serikali iliamua kuajiri vijana 500 wa BBT ambao wamesambazwa katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Pwani na Tanga kuongeza tija kwenye uzalishaji wa korosho na kufikia lengo la kuzalisha tanki 700,000 2025/2026 kutoka tani 528,262.23 zilizozalishwa 2024/2025.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button