80%Watanzania wanatumia nishati ya kuni na mkaa

TANGA: Takwimu zinaonyesha zaidi ya asilimia 80 ya familia zinatumia nishati ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia, kitendo ambacho kinachangia sana mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa afya Ummy Mwalimu wakati wa hafla ya  awamu ya pili ya kukabidhi vitendea kazi ikiwemo mitungi ya gesi  kwa wanawake wajasiriamali 311 waliopo jijini Tanga.

Licha ya kwamba bado gharama ya matumizi ya gesi kimsingi kuwa chini kuliko kuni na mkaa, serikali inafanya mazungumzo na kampuni za gesi ili kuona uwezekano wa mtumiaji kuweza kununua gesi kwa kadri anavyotumia kama ilivyo kwa luku.

Hata hivyo ameupongeza mradi wa Mwanamke Shujaa unaoendeshwa na Kampuni ya Coca-Cola wenye lengo la kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutumia nishati mbadala kwenye shughuli zao za kujiongezea kipato.

“Nimependa ubunifu wa Coca-Cola ambapo leo tumeona kila mwanamke akipewa mtungi wa gesi, jiko la gesi na meza yake, sanduku la soda pamoja na mavazi ya kuhudumia wateja,”alisema Waziri Ummy.

Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola  Unguu Salum amesema mradi wa Mwanamke Shujaa  umeweza kunufaisha wanawake zaidi ya 6700 katika kipindi Cha miaka mitatu .

“Mradi wa Mwanamke Shujaa ni programu endelevu ya kumuendeleza mwanamke, tulifanya utafiti na kugundua kuwa maisha mengi ya watanzania yanawezeshwa na wanawake waliojiajiri na idadi kubwa wapo katika sekta ya mama lishe ambapo Kwa Tanga pekee kukiwa na wanufaika zaidi ya 1731″amesema Unguu.

Habari Zifananazo

Back to top button