Bajeti imezingatia nyongeza ya mishahara

DODOMA; WAZIRI WA Fedha, Dk Mwigulu Nchemba amesema bajeti ya serikali mwaka 2025/26 imezingatia nyongeza ya mishahara iliyotangazwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan, Mei Mosi mwaka huu.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2025/26 bungeni leo Juni 12, 2025, Waziri Nchemba, amesema watumishi watarajie kuona maokoto hayo kwenye mishahara yao kuanzia Julai.

“Mheshimiwa Dk  Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliongeza kima cha chini cha mshahara kutoka shilingi 300,000 hadi shilingi 370,000, sawa na ongezeko la asilimia 23.3, kwa lengo la kuongeza motisha na kuwezesha watumishi wa umma kumudu gharama za maisha.

“Aidha, kwa kutambua mchango wa watumishi wa umma katika ujenzi wa Taifa letu na kwa kuwa ni Mama mwenye upendo na anayejali, tarehe 1 Mei, 2025 katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, Mheshimiwa Rais, ameongeza tena kima cha chini cha mshahara kutoka shilingi 370,000 hadi shilingi 500,000, sawa na ongezeko la asilimia 35.

“Napenda kulihakikishia Bunge lako Tukufu kuwa bajeti hii imezingatia nyongeza hiyo. Hivyo, tutarajie kuyaon

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button