Simba wamejipanga bwana!

DAR ES SALAAM: KLABU ya Simba SC imerejea rasmi katika uwanja wa mazoezi kuanza maandalizi ya mchezo muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika  dhidi ya Esperance ya Tunisia, huku uongozi wa klabu hiyo ukiwataka mashabiki wake kuwa watulivu kuhusu masuala ya usajili.

Simba ilikuwa Zanzibar, ambako Alhamisi ilitolewa nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kufungwa bao 1-0 na Azam FC.

Kwa mujibu wa taarifa ya Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ally Dar es Salaam leo, kikosi hicho tayari kimeanza mazoezi kwa lengo la kujiweka sawa kuelekea mchezo huo wa Kundi D utakaochezwa ugenini nchini Tunisia Januari 23, mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Ally aligusia shauku kubwa iliyopo miongoni mwa mashabiki wa Simba kuhusu taarifa za usajili, akibainisha kuwa suala hilo linafanyiwa kazi kwa umakini mkubwa na viongozi wa klabu kwa kushirikiana na benchi la ufundi.

“Tunafahamu shauku kubwa ya Wana Simba kusikia taarifa za usajili za klabu yao, lakini nichukue nafasi hii kuwaomba wawe watulivu nyakati hizi ambazo viongozi wetu wanafanyia kazi mapendekezo ya benchi la ufundi,” aliongeza.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button