Elimu kutolewa sekta ya uwekezaji

DAR ES SALAAM; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais MIpango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo, amesema serikali inakusudia kutoa elimu kuhusu sekta ya uwekezaji, hasa kwa Watanzania ili kuhakikisha miradi mingi inamilikiwa na wazawa.

Profesa Mkumbo ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam, wakati akizindua kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani ambayo imelenga kufanyika nchi nzima katika kipindi cha siku 60.

Pamoja na hayo amewataka Watanzania wanaomiliki ardhi kuzielekeza katika uzalishaji, ili ziweze kuwaingizia kipato na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Gilead Teri  ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), amesema mamlaka hiyo imejiwekea malengo makuu mbalimbali ikiwemo kufikia miradi 1,500.

Kwa upande wake Meneja Mawasiliano na Uhusiano Kampuni ya Sukari ya Kilombero Victor Byemelwa, ameishukuru serikali kupitia mamlaka ya uwekezaji na maeneo maalumu ya kiuchumi kwa kuendelea kutatua kero zao.

Ziara hiyo inatarajiwa kuanza Januari 17, 2026 katika mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani, huku elimu itakayotolewa ni pamoja na sekta za kipaumbele zilizoainishwa kwenye Dira ya Taifa 2050.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button