Mawaziri kuwasilisha utekelezaji kila miezi 3

DODOMA; SERIKALI imesema imeandaa mfumo wa ufuatiliaji na upimaji unaozingatia kupima matokeo na uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Prof Kitila Mkumbo, ametoa kauli hiyo bungeni leo akiwasilisha nyenzo tatu zitakazowezesha kuanza utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Nyenzo hizo ni Mpango Elekezi wa Muda mrefu wa miaka 25 (2026/27 hadi 2050/51), Mpango wa Nne wa Maendeleo wa miaka mitano (2026/27 hadi 2030/31) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2026/27.
“Serikali imejipanga kuimarisha mfumo wa usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa programu na miradi ya maendeleo itakayopitishwa na Bunge lako tukufu.
“Tumeandaa mfumo wa ufuatiliaji na upimaji unaozingatia kupima matokeo na uwajibikaji (Results-based Monitoring, Evaluation, Learning and Accountability Framework).
“Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumo mpya wa ufuatiliaji na upimaji umejengwa katika nguzo tatu, ambazo ni: kuainisha vipaumbele bayana na kwa uwazi kwa kila sekta (prioritisation); nidhamu ya utekelezaji (discipline of implementation); na uwajibikaji (accountability). Katika kutekeleza mfumo huu, hatua zifuatazo zitatekelezwa:
“Kila sekta inayotekeleza programu na miradi ya maendeleo itapaswa kuweka malengo na viashiria vya utekelezaji vinayopimika, pamoja na mikakati mbalimbali itakayofanyika kufikia malengo hayo;.
“ Taarifa ya utekelezaji itawasilishwa kwa Tume ya Taifa ya Mipango kila mwezi;
“ Mawaziri watawasilisha taarifa za utekelezaji kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu kila baada ya miezi mitatu.
“Tume ya Taifa ya Mipango itatoa taarifa ya utekelezaji wa programu na miradi ya maendeleo kwa umma kila mwaka kupitia tukio la wazi.
“Kwa kuzingatia Kifungu cha 7 cha Sheria ya Tume ya Mipango, 2023, Tume itakuwa na mamlaka ya kuitisha vikao vya viongozi wa juu wanaosimamia utekelezaji wa programu na miradi ya maendeleo kwa lengo la kuratibu uchambuzi wa changamoto za utekelezaji na kusukuma utekelezaji wa suluhu zilizokubalika ili kuondoa vikwazo vya utekelezaji, kuboresha uratibu na kupata taarifa kwa wakati mwafaka,” amesema.




QQ88 mang đến nền tảng giải trí trực tuyến được tối ưu hiệu suất, giúp người dùng truy cập nhanh, thao tác mượt và trải nghiệm ổn định.