Dk Mwigulu: Serikali kununua matrekta 10,000

WAZIRI Mkuu Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali imepanga kununua matrekta 10,000 na kuanzisha vituo jumuishi 1,000 vya huduma za zana za kilimo katika ngazi ya Kata, hatua itakayoongeza tija, kupunguza gharama na kuwapa wakulima muda zaidi wa kushiriki shughuli nyingine za kiuchumi.
Ametoa kauli hiyo leo Februari 3, 2026 wakati akifungua Mkutano wa Kwanza wa Kikanda wa Afrika wa Matumizi Endelevu ya Zana za Kilimo unaofanyika, Dar es Salaam unaolenga kuweka msingi wa ushirikiano wa kikanda katika kuendeleza Ajenda ya Mfumo wa Zana Endelevu za Kilimo Barani Afrika (F-SAMA).

Dk Mwigulu amesema ni muhimu kuimarisha uwekezaji katika zana za kilimo rafiki kwa mazingira na zinazozingatia mabadiliko ya tabianchi.
SOMA: Wakulima Kongwa wakabidhiwa trekta 15
“Zana hizi zinapaswa kupunguza uzito wa kazi, kuongeza tija, kupunguza upotevu wa mazao, na wakati huo huo kulinda mazingira kwa kutumia teknolojia zinazohimili athari za tabianchi kama ukame na mabadiliko ya misimu.”

“Tunapaswa kuhakikisha ushiriki mkubwa na wa makusudi wa Sekta Binafsi katika uzalishaji, usambazaji na utoaji wa huduma za zana za kilimo. Serikali zetu zinapaswa kuweka mazingira wezeshi ya sera, sheria na vivutio vya uwekezaji ili Sekta Binafsi iweze kushiriki kikamilifu, kuongeza upatikanaji wa zana za kilimo, na kupunguza gharama kwa wakulima,” amesema.

Waziri Mkuu amesema kuwa ni lazima kuwawezesha vijana na wanawake kushiriki kikamilifu katika biashara, ubunifu na utoaji wa huduma za zana za kilimo kwa kuwa ni kundi lenye nguvu kazi, ubunifu na uwezo wa kuleta mabadiliko ya haraka endapo litapatiwa mafunzo, mitaji, teknolojia na fursa za masoko.

Amesema uwezeshaji wa makundi hayo ni msingi wa maendeleo jumuishi na endelevu.
“Uwezeshaji huu unapaswa kupimwa kwa viashiria mahsusi vya ajira, uanzishwaji wa biashara endelevu, na ushiriki wa vijana na wanawake katika minyororo ya thamani ya zana za kilimo,” amesisitiza Dk Nchemba.

I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com
I make up to $90 an hour working from my home. My story is that I quit working at Walmart to work online and with a little effort I easily bring in around $40h to $86h… Someone was good to me by sharing this link with me, so now i am hoping i could help someone else out there by sharing this link…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com
Wakugawana vya kwake haeleweki Tanzania – Tukagawane Kutokueleweka kwake 【Kilimo ni uti wa mgongo